SHILOLE AMTETEA SERENGETI BOY WAKE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/shilole-amtetea-serengeti-boy-wake.html
MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa
kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametetea maisha yake ya
kimapenzi na Nuh Mziwanda, akisema madai kwamba ni kijana mdogo kuliko
yeye, siyo kweli kwani wanalingana umri.

“Mimi na Mziwanda wangu tunalingana kiumri lakini nawashangaa sana wanaonisema kila siku eti ninatembea na Serengeti boy, jamani mpenzi wangu siyo mdogo kwangu, tunalingana umri, ninampenda na yeye ananipenda, hatujali maneno ya watu,”alisema Shilole. Katika kuonyesha mapenzi yake kwa mwanadada huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Mziwanda amejichora tattoo yenye jina la msanii huyo, ambalo haliwezi kufutika.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA