SIPENDI KUZINI NITAOLEWA TENA - KHADIJA KOPA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/sipendi-kuzini-nitaolewa-tena-khadija.html
Malkia
ya mipasho Tanzania Bi Khadija Kopa amevunja ukimya na kuweka wazi kuwa
ataolewa baadae sababu hapendi vitendo vya uzinifu,Khadija Kopa amesema
hayo leo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV

katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka saa Nane za mchana.
Khadija Kopa amefunguka na kusema kuwa baada ya mume wake kufariki na muda kupita itambidi aolewe tena maana hawezi kuwa mzinifu hivyo atafuata taratibu za imani yake na kufunga ndoa ili awe mke halali na aepuke uzinifu."Kwa kuwa mimi ni Muislamu safi hivyo Baadae nitaolewa kwasababu sipendi kuzini"
Mbali na suala la kuolewa Malkia wa mipasho amekana tuhuma zilizopo mtaani kuwa anapenda sana dogo dogo maarufu kama Serengeti Boys na kusema kuwa yeye anampenda mtu anaempenda na yule ambae anakuwa na makubaliano nae tena kwa maelewano na si kama ambavyo watU wanakuwa wakisema kuwa anatoka na watoto wadogo.
"Ni kweli mwenyewe nasikia haya mambo lakini sio kweli mimi sipendi Serengeti Boys ila nampenda anae nipenda kwa maelewano,hivyo mkae mkijua wazi kabisaa.Khadija Kopa mimi sipendi watoto wadogo ila nampenda mtu mzima mwenzangu mimi sio shuga mami wale wanaopenda kulelewa wasinikaribie kabisa maana mimi siyo aina yao".
MUZIKI WA TAARABU
Malkia wa mipasho Tanzania amesema kuwa katika muziki wa taarabu kwa sasa kuna tatizo kubwa moja wasanii wa taarabu hawana umoja na hivyo hali hiyo inafanya muziki wa Taarabu na wasanii kutokuwa na nguvu ya pamoja,pia Kopa alisema kuwa kumekuwa na tatizo kwa wasanii wa sasa wa taarabu kutaka umaarufu ambao hata wakongwe hawakuwahi kuwa nao hivyo inapelekea muziki huo kushuka hadhi yake kutokana na ukweli kwamba inafika mahali huo umaarufu wanaokuwa wakiuhitaji unashusha maadili na kupotosha watu.
"Wasanii wa kizazi cha sasa katika Taarabu wengi wao wanajifurahisha hawapo kikazi wanataka kuonekana na kupenda ustaa ambao hata sisi tulowatangulia hatuna hapo ndio tatizo na wanapelekea kushuka heshima ya muziki wa Taarabu na kiuonekana muziki usiona na haiba na nidhamu."
SABABU YA KUWA MREMBO MPAKA SASA
Malkia wa mipasho Khadja Kopa ameweka wazi sababu inayomfanya siku zote kuonekana mrembo kuwa anamshukuru Mungu lakini pia hapendi kujifuja,hapendi zinaa wala makrimu,mbali na hivyo anadai kuwa hatumi kilevi chochote maana hivyo ndivyo adui mkubwa wa uzuri wetu asili.
"Mungu mkubwa lakini sipendi kujifuja sipendi zinaa wala makrimu pombe hivyo ndio maadui wa uzuri wetu,lakini mwenyewe najikubali najiamini ndio mana situmii mkorogo mwanamke kujiam bwana."
Malkia wa mipasho Tanzania amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio yake katika muziki wa Taarabu mpaka leo ni kwakuwa anapenda kwenda na wakati hivyo hakuna mtu anaweza kumtingisha kwa kuwa hata hao chipukizi wanamsona na kumuelewa vizuri ndio maana siku zote wataendelea kumuogopa na kumheshimu katika fani.Mimi mwenyewe nakwenda na wakati ndiomaana sichuji na wananijuwa na wananiogopa pia.

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA