MGANGA ANASWA GUEST NA WAKE ZA WATU USIKU WA MANANE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mganga-anaswa-guest-na-wake-za-watu.html
Ama kweli uswazi hakuishi vijimambo! Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam
Tukio
hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia
Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa
ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.Kwa mujibu wa mashuhuda,
jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya
mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.
Ilidaiwa
kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja
baada ya mwingine.Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo
amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali
ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la
kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka
na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani.
Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo
kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo
yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali.
Kiliendelea kudai kwamba, sangoma
huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia
bila kukosea hivyo kuwachanganya na kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa
masuala hayo.
Ilisemekana kwamba uzalendo
ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya kilinge cha sangoma
huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha funguo."Haaamadi!"
alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa
vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa
kumfanyia ‘amshaamsha’.
Ilidaiwa kuwa Huruka alishindwa
kujizuia, akagonga mlango kwa hasira ambapo sangoma alivaa 'chapchap' na
kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana uso kwa uso, Huruka
alitunishiana misuli na sangoma huyo wakataka kuzichapa lakini jamaa
akaona amchukue mkewe na kutimka naye.
Baada ya mke wa Huruka kuokolewa
kufanyiwa ukenge, mwanamke mwingine wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye
alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa amekalishwa kama
alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma huyo.
Akizungumza na Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) ya Global Publisher ambayo ilifika eneo hilo usiku baada ya
kutonywa na chanzo chake, Tabu alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo
baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia gesti hiyo.
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo.
Baada ya kutokea kwa mtiti huo,
Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj Neto, wanawake
waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo, Ebenezer
Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo.
Katika hali ya kushangaza mke wa Tabu
alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka kumpiga mganga wake ambaye alikuwa
akitaka kummalizia matatizo huku wanawake wengine wakiwaomba radhi waume
zao na kudai walirubuniwa.
Akizungumizia mkasa huo mke wa Tabu
alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani ambapo alimwita majina
yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo akaanza kumtajia matatizo
yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia mama huyo huko aliko ana
tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli ndipo alianza kumuamini.
MWISHO WA SAKATA
Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa
nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti
hiyo alimtaka mganga huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia
yake ya kubadilisha wanawake.
Kwa upande wao, polisi walimshikilia
sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na
wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumu.
>>>>>>GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu. LIKE HAPA