TAARIFA MPYA KUHUSU GOLIKIPA WA MEXICO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/taarifa-mpya-kuhusu-golikipa-wa-mexico.html
Katika
michuano ya kombe la dunia kumeibuka wachezaji wengi ambao wameonyesha
uwezo mkubwa kiasi cha kuteka hisia za watu wengi, mmoja wapo ni
golikipa wa Mexico Guillermo Ochoa.Golikipa huyu alionyesha uwezo mkubwa
katika mechi alizoichezea Mexico kwenye michuano ya kombe la dunia
inayoendelea nchini Brazil, kabla ya timu yake kutolewa na Uholanzi
katika hatua 16 bora – lakini pamoja na kuondolewa kwa timu yake bado
uwezo wake umeacha gumzo kubwa sana kwenye michuano hii.
Uwezo
aliouonyesha Ochoa ulipelekea kuzuka kwa taarifa kwamba golikipa huyo wa
Mexico aliumbwa akiwa na vidole sita vya mkononi. Zikatolewa mpaka
picha kupitia vyombo vya habari mbalimbali ambavyo vilimuonyesha Ochoa
akiwa na vidole sita.
Lakini
ukweli ni kwamba kipa huyo ambaye kwa sasa anawindwa na vilabu vingi
hana vidole sita. Picha zilizoonyeshwa na kusambazwa kwenye vyombo vya
habari ni za kutengeneza.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA