TAZAMA PICHA KIJANA WA MIAKA 17 ANG'OLEWA MENO 232

Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba.
Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.
Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo.

Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia".
Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili.
Ashik sasa ana meno 28.

Madaktari walio mfanyia opasuaji wa kuondoa meno
 "Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware.
"Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.

Muonekano wa meno baada ya kutolewa kwenye kina cha kijana huyu.
"Tulivyopasua tu, meno madogo madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na tulipoyahesabu, yalifika meno 232." Amesema daktari huyo.


kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

MATUKIO 9068574664338237104

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item