TIMBWILI GESTI, WAJOMBA WAZICHAPA KAVU KAVU KISA MKE WA MTU
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/timbwili-gesti-wajomba-wazichapa-kavu.html
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi
Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana
kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin asizidi kumjeruhi mjomba wake.
OFM KAZINI, AIBU!
Kufuatia taarifa hiyo, mkuu wa zamu wa OFM
aliwaagiza mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao
walitumia muda usiozidi robo saa kutoka walipokuwa kufika eneo la tukio
ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili
zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama
alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!
Mjomba akiwa chumba cha gesti mara baada ya mkong'oto 'hevi' kutoka kwa mpwa wake.
PICHA ZA TUKIO
Mapaparazi wetu bila kuzubaa nao walianza
kuchukua picha za tukio hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea,
Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili
wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka
nyumbani kwa mke wake.
MKE ATIMKA KINYEMELA
Katika hali ya kushangza, wakati
wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na
kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.
...Mjomba taratiiibu 'akirejesha' mavazi mwilini mwake.
MLINZI WA GESTI
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na
mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana) ambaye alitumia mabavu na
kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
MJOMBA MTU AGOMA KWENDA POLISI
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania
waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa
wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema
mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
CHONDECHONDE KELVIN
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia
tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia
kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na
kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe. MJOMBA ‘AJIKOMITI’ KIMAANDISHI
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa
gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye
‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi
laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Sehemu ya nyaraka ikionyesha mjomba 'akijikomiti' kimaandishi.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa
mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki
tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku
inayofuata.
MGONI AGEUKA NA KWENDA KUFUNGUA KESI
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati
tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi
(jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe
Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa sababu kisa hiki kinadaiwa kufikishwa
polisi na Joseph, magazeti pendwa ya Global yataendelea kukifuatilia ili
kujua mwisho wake. Endelea kusoma.
Credit gazeti la Ijumaa via GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA