TETESI ZA USAJILI MAGAZETI YA LEO BARANI ULAYA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/tetesi-za-usajili-magazeti-ya-leo.html
Meneja mpya wa Manchester
United Louis van Gaal ameambiwa kuwa anaweza kutumia kiasi chochote cha
fedha kusajili wachezaji wapya Old Trafford na hata kuvunja rekodi za
uhamisho (Guardian), Man U Pia wametajiwa kuwa wanaweza kuendelea
kumsaka Angel Di Maria, 26, kufuatia Real Madrid kumsajili kiungo
mshambuliaji James Rodriguez, 23, kutoka Monaco (Independent), Arsenal
wamekubali ada ya uhamisho ya pauni milioni 3 kumsajili kipa wa David
Ospina, 25 kutoka Nice ya Ufaransa (Guardian), boss wa Liverpool Brendan
Rodgers anataka kumsajili beki wa kulia Javier Manquillo, 20, kutoka
Atletico Madrid kwa mkopo. Mchezaji huyo anawindwa pia na Arsenal (Sun),
Atletico Madrid wanawanyatia wachezaji wawili wa Arsenal, Santi Cazorla
na Nancho Monreal (Daily Telegraph), Arsenal wamerejea kumyatia kiungo
wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22, baada ya mazungumzo ya
kumchukua Sami Khedira wa Real Madrid, 27, kusuasua (Daily Star),
Tottenham na Arsenal wanaonesha nia ya kumsajili kiungo mshabuliaji
Douglas Costa, 23, kutoka Shakhtar Donetsk. Mchezaji huyo kutoka Brazil
amekataa kurejea Ukraine kutokana na matatizo ya kisiasa katika nchi
hiyo (Independent), mshambuliaji Divock Origi, 19, amesafiri kwenda
Marekani kukamilisha usajili wake wa Liverpool, lakini atabakia Lille
kwa msimu ujao (Daily Express), uwezekano wa Didier Drogba, 36, kurejea
Chelsea huenda kukasababisha Romelu Lukaku kuondoka Darajani, na huenda
akaenda Everton (Daily Telegraph), Everton wameripotiwa kukaribia
kumsajili David Henen, 18, kutoka Anderlecht (Liverpool Echo), Inter
Milan wako makini kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier
Hernandez, baada ya kuambiwa na Manchester City kuwa Stevan Jovetic, 24,
hauzwi (Sun), Hull City wanazungumza na beki wa kimataifa kutoka
Cameroon Jean-Armel Kana-Biyik, 25 kutaka kumsajili kutoka Rennes ya
Ufaransa (Sky Sports), Lionel Messi, 27, 'alitishia' kujiunga na Arsenal
msimu uliopita, wakati akizungumzia mkataba wake mpya na Barcelona
(Daily Mail), Luis Suarez, 27, ameukimbia mji wa Barcelona, kuwaepuka
waandishi wa habari wanaomfuatilia kwa karibu (Daily Star), Manchester
United wanajiandaa kutoa pauni milioni 39 kumchukua Arturo Vidal, 27,
kutoka Juventus (Tuttosport), klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani
imefuta mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas
Bendtner, 26, kwa sababu mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa (Le
Figaro), meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp ametupilia mbali
tetesi kuwa beki Mats Hummels, 25, anakwenda Manchester United, na
kiungo Marco Reus, 25 anakwenda Bayern Munich (Bild), Atletico Madrid
wanashindwa kutoa pauni milioni 13 wanazotaka Chelsea kumsajili Fernando
Torres, 30, licha ya kuwa meneja Diego Simione kutaka sana kumchukua
(AS).
Tetesi kwa hisani ya Salim kikeke. Cheers!
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA
Tetesi kwa hisani ya Salim kikeke. Cheers!
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA