TUNDA MAN APIGIWA SIMU YENYE NAMBA YA AJABU NA KUPIGWA SHOTI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/tunda-man-apigiwa-simu-yenye-namba-ya.html

Tunda Man ambaye pia ni miongoni mwa watu wanaounda kundi la Tip Top
Connection Jioni ya July 28 amepata simu hiyo ambayo amedai kwake ilikua
ni mara ya kwanza kupigiwa kwani namba hizo hajawahi kuziona zikimpigia
kabla.
’Nilikua nafuturu jana jioni wakati naendelea kufuturu nikapigiwa simu
namba sikua nazijua kwani zilikua za maajabu tu,sikupokea,ilipiga kama
mara 30 hivi’
‘Baadae nikapokea na kisha nikaiweka mbali kidogo na mimi wakati nasema
hallow ghafla kitu kama shoti ya umeme kikaanza kutembea kwenye viganja
mpaka kwenye mkono nikakosa nguvu kabisa nikawaambia jamani nipelekeni
hospital’
‘Tukaenda hospital ya Serikali hapo Palestina,Dokta akasema huu ugonjwa
tangu ameanza kutibia watu hajakutana nao ni mara yake ya kwanza hivyo
matibabu aliyokuwa akinipatia ni kama ya mtu aliyepooza ghafla’
‘Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri ingawa kuna dawa nimepewa
zingine nameza mara 2 kwa siku na vidonge vingine ni mara 3 kwa siku pia
nimechomwa sindano’
Hii ndiyo namba iliyompigia Tunda
