WINGA WA CHELSEA MOHAMED SALAH KUACHANA NA SOKA NA KUJIUNGA JESHI

MUSTAKABALI wa Mohamed Salah katika klabu ya Chelsea upo shakani, baada ya kutakiwa kurejea nyumbani kwao, Msiri kuchukua mafunzo ya jeshi.

Salah, aliyehamia Stamford Bridge kutoka Basle ya Uswisi Januari mwaka huu, ameruhusiwa kuishi England kwa kigezo cha kushiriki masomo. Pamoja na hayo, usajili wake umesitishwa na Wizara ya Elimu ya Juu Misri, tovuti ya soika ya www.kingfut.com imesema, maana yake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaweza kurudi nchini mwao.
Jeshini kwanza; Mo Salah anatakiwa kurudi nyumbani kupata mafunzo ya Jeshi Ikiwa Salah, aliyeichezea Chelsea mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Wimbledon jana atatakiwa kurejea nyumbani, hataruhusiwa kuondoka tena Misri hadi akamilishe mafunzo ya kijeshi, yanayochukua mwaka mmoja hadi mitatu. "Salah ameelesea namna alivyoshitushwa juu ya uamuzi huu," amesema Mkurugenzi wa timu ya taifa ya Misri, Ahmed Hassan.
"Ameniambia anajaribu kuiwakilisha Misri katika njia nzuri zinazowezekana. Na haya ndiyo matokeo yake kutoka kwa nchi yake?' Kikao kinatarajiwa kufanyika baina ya FA ya Misri, benchi la ufundi la timu ya taifa na Waziri wa Elimu ya Juu, kutafuta suluhisho.

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

MICHEZO 4926599565052173928

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item