ZA MWIZI AROBAINI! DEREVA BODABODA ALIMANUSURA ATOLEWE UPEPO BAADA YA KUKWAPUA SIMU
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/za-mwizi-arobaini-dereva-bodaboda.html
Za mwizi arobaini! Ule mchezo wa kukwapua vitu na
kukimbia umemtokea puani dereva wa pikipiki almaarufu bodaboda
aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) ambaye amenusa kifo baada
ya kukwapua simu ya bei mbaya ya mrembo aitwaye Zaituni Hamisi.
Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za kisheria.
Credit GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA
Dereva wa bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu.
Tukio hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita
maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda
huyo alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma
wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.
Dereva wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa
kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati
nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na
kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye kuingia mtaroni.
Raia wakiitoa bodaboda kutoka mtaroni.
Ndani ya dakika sifuri, yule mkwapuaji alitoka nduki huku akimwacha bodaboda huyo aliyekiona cha moto.
Zaituni Hamisi (kulia) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha bodaboda.
Alisema ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo cha kufa
mtu na wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba ya
watu.Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua
mafuta ya petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye
alikuwa akijitahidi kutuliza ghasia hizo.Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za kisheria.
Credit GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA