MAJONZI: MUIMBAJI MWINGINE WA INJILI AFARIKI DUNIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/zikiwa-ni-takribani-wiki-tatu-tangu.html
Zikiwa
ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini
kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi,
taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa
injili Orida Njole amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya
Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida
ambaye mpaka umauti unamfika mchana wa leo ilikuwa bado haijajulikana
nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa damu sana, mpaka umauti
unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani tu wapitaji'
huku kwa mujibu wa watu waliomfahamu marehemu wameeleza kwamba alikuwa
mtu mchangamfu wakati wote wakati wa uhai wake na kwamba wamepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!
![]() |
Picha ya mbele ya álbum ya marehemu Orida Njole. |
![]() |
Marehemu Orida akiwa na mtoto yatima katika kituo cha Tosamaganga Iringa alipotembelea kituoni hapo |