AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA WAKATI MMOJA HUKO MWANZA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/ajifungua-watoto-wanne-kwa-wakati-mmoja.html
Watoto wa Tecra waliozaliwa wakiwa ni wanne huku mmojawapo ambaye hakufunuliwa uso akiwa amefariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa
Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Proscovia Leopod akimhudumia bi Tecra baada ya kujifungua
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Tecra Kazimili(24) mkazi wa Lubili katika wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza amjefungua watoto (4) kwa wakati mmoja huku mtoto mmoja wa kiume akifariki muda mfupi baada ya mama huyo kujifungua.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo si la kawaida mama Tecra alisema hii ni mara yake ya nne kujifungua lakini ni mara yake ya kwanza kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja.