ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUMWAGIWA UJI NA BOSI WAKE KWA WIVU WA MAPENZI!
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/anusurika-kufa-baada-ya-kumwagiwa-uji.html

MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka),
amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri
yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian ameifahamisha FikraPevu
kuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na
mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana
na matibabu anayoyapata hospitalini hapo.

Akizungumza na FikraPevu leo Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.

Majeruhi,
Jackline Lasway, akiwa amelazwa katika wodi ya wanawake katika
Hospitali ya mkoa wa Singida, baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa uji wa
moto wakati akiwa dukani kwa bosi wake katika Manispaa ya Singida
Pendo amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 9, 2014
saa nane mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina
la, Charles Kamnde.
Amesema akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani
hapo, gafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto
na kuwa alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka
kujiokoa ili usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la
kulia na mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa
kisu kutaka kumchoma kifuani.
“Mimi sikuwa na ugomvi naye wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na
kunifanyia vile jana, maana kama ni kazi mimi ninafanya kulingana na
maelekezo kutoka kwa bosi wangu Chale lakini sijui kilichomfanya
afikirie kunifanyia huu unyama” alisema.
Aidha, amesema katika purukushani za kujiokoa kuwa asichomwe kisu
hicho, alifanikiwa kumkamata mkono mwanamke huyo na kupiga kelele za
kuomba msaada ambapo watu walifika na kumwokoa baada ya muda mchache
ambapo alichukuliwa na bosi wake hadi Kituo cha Polisi mjini Singida na
kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na kupelekwa katika hospitali hiyo
ambako amelazwa huku akiwa ma majeraha mwilini.
Kwa upande wake, mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani maelezo
aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na FikraPevu baadhi
ya majirani wa familia hiyo, wameonyesha masikitiko yao juu ya tukio
hilo na hatua ya mwananmke huyo kummwagia uji msichana huyo huku
wakihusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi baina ya mfanyakazi huyo na
mume wa mtuhumiwa.
“Kama aliona kama kuna sehemu kamkosea angemuonya au kama ameshindwa
kueleweka basi angemshitaki hata polisi kwani kitu alichokifanya
hakiendani na haki za binadamu kwakuwa ni kumdhalilisha huyu msichana
ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato chake na
familia yake.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuwa wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na mara
baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Chanzo FIKRAPEVU
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA