APIGWA RISASI KWAPANI



  Mke wa Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wafugaji la Pingos Forum, Edward Porokwa, Flora Porokwa aliyepigwa risasi.
MKE wa Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wafugaji la Pingos Forum, Edward Porokwa, Flora Porokwa (37), mkazi wa Sakina Kwaidi amepigwa risasi na watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi.Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo risasi hiyo alipigwa kwapani na kwenda kutokea mgongoni na kulazimika kuendesha gari umbali wa kilometa moja akiwa na risasi mwilini. 


Majeruhi huyo ambaye  amelazwa katika Hospitali ya Seliani jijini hapa, alionesha ujasiri wa hali ya juu baada ya kumudu kuendesha gari hilo huku watu hao wawili waliokuwa wamepanda bodaboda wakiendelea kumfuatilia hadi alipofika nje ya nyumba yake ambapo aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa anasubiri kufunguliwa geti la kuingia ndani. Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo, majeruhi huyo alisema tukio hilo lilimtokea jioni ya saa moja kasoro katika Barabara ya Arusha - Namanga eneo la Kwaidi ambapo watu hao walimvamia ghafla na kulizuia gari lake kwa mbele wakitumia  pikipiki hiyo.


Jeraha la mgongoni alilopata Flora Porokwa.
Alisema mmoja wa watu hao alimfuata na kushika kitasa cha mlango wa mbele na kujaribu kufungua lakini mlango haukufunguka. Ndipo mwanamke huyo alipoamua kushusha kioo cha mlango ili aweze kumsikiliza, lakini ghafla jambazi huyo alichomoa bastola na kumpiga risasi kwapani.

“Kwenye gari sikuwa na fedha, sijui kama walilenga kunipora au kuna tatizo lingine. Nikiwaona naweza kuwakumbuka kwa sura ila siwajui, sikuwahi kuwaona kabla,’’
alisema mwanamke huyo na kuongeza kuwa:

“Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na kifo kwani dhamira yao ilikuwa kuniua.”
Majeruhi huyo ambaye hali yake bado siyo vizuri, alitoa rai kwa jeshi la polisi mkoani Arusha kuwasaka watu hao kisha kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. 

Hadi sasa tukio hilo halijafahamika undani wake kama watu hao walilenga kupora fedha au ni  kisasi, kwani kabla ya tukio hilo kuna taarifa kwamba hata mumewe, Porokwa aliwahi kupigwa risasi na watu wasiojulikana. 

Jirani mmoja wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema wamesikitishwa mno na tukio la mwenzao kupigwa risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo. 

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

MATUKIO 5473348091641191025

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item