AUAWA KIKATILI KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO MOROGORO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/auawa-kikatili-kisha-mwili-wake.html
Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika
mara moja ameuwawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu
wasiofahamika katika eneo la mkundi manispa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema wameshuhudia
kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kummwagia
mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi
kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.
Wananchi wakazi wa kata ya mkundi wamesema hilo sio tukio la kwanza
kutokea kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya
sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu
kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru
na vyombo vya sheria pasipo kuchukuliwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo .
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA