MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA NA NJEMBA LENYE MIAKA 30
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/mtoto-wa-mwaka-mmoja-abakwa-na-njemba.html

Mtoto
wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota
wa Sokoni One jijini hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa
eneo hilo.Tukio
hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo
anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama
yake usiku wa manane.
Akizungumza na
paparazi wetu, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la
Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa
jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda
kwenye kikundi cha akina mama.
Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata
hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.“Lakini
kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na
mtoto wangu akaniambia nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa
niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema
mwanamke huyo“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi,
nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha
kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu
ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku
damu zikimtoka.
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto
wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa
za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema
mama huyo.
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo
hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti
shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo
walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo
kwenye vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi
cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na
kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na
kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye
namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada
ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano .