DEREVA BODA BODA ASAKWA KWA KUUA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/dereva-boda-boda-asakwa-kwa-kuua.html
Jeshi
la polisi Mkoani Iringa linamtafuta dereva wa pikipiki kwa tuhuma ya
kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu kwa ajali ya barabarani kisha
kukimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP
Ramadhani Mungi amesema Mfaume Kilangi ambaye pia ni mwenyekitio wa
kijiji cha Idodi wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa akiwa
anaendesha pikipiki ambayo haijafahamika namba zake za uasjili ilimgonga
na kusababisha kifo cha Laurent Kafwela umri miaka 40.
Aidha
ameongeza kuwa marehemu amefariki muda mfupi akiwa anakimbizwa katika
hospitari ya Mapogoro wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa wa Iringa na chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa kutochukua
tahadhari kwenye makazi ya watu.
Hata
hivyo Kamanda Mungi amesema ajari hiyo imetokea katika eneo la Mapogoro
katika barabara ya Idodi-Tagamenda wilaya ya Iringa Vijijini pia ametoa
wito kwa wamiliki na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa
kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajari zinazoweza
kuepukika.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA