LIBERIA KUPATA DAWA MPYA KUPAMBANA NA EBOLA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/liberia-kupata-dawa-mpya-kupambana-na.html

Liberia itapatiwa dawa za majaribio - ambazo hazijafanyiwa majaribio, Zmapp, kujaribu kutibu watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola, imesema serikali ya Liberia. Hatua hiyo imekuja baada ya ombi kutolewa kwa Marekani na Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, imesema serikali. Habari hizi zimekuja wakati wataalam wa maadili ya kitabibu wakikutana mjini Geneva, kutazama jinsi ya kutumia dawa mpya kama hizo. Shirika la Afya Duniani, WHO, ambalo limeandaa mkutano huo, limesema watu wapatao 1,013 wamekufa Afrika Magharibi kutokana na Ebola.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA