ABIRIA WANUSURIKA KIFO WAKISUBIRI USAFIRI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/abiria-wanusurika-kifo-wakisubiri.html
Gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU likiwa eneo la kituo cha mabasi.
ABIRIA
waliokuwa katika kituo cha mabasi eneo la Quality Plaza jijini Dar
wakisubiri usafiri wamenusurika kifo baada ya gari aina ya Toyota Raum
lenye namba za usajili T483 CMU, kuhama njia katika barabara ya Nyerere
na kuparamia kituo hicho.
Dereva wa gari lililopata ajali ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiongea na simu baada ya kunusurika kifo.
Dereva
wa gari hilo mwenye asili ya Kihindi ambaye jina lake halikufahamika
mara moja alishindwa kulimudu ndipo lilipovuka ukingo unaotenganisha
barabara hiyo na kuhamia upande wa pili kisha kuparamia kituo cha
abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa
Tairi likiwa limepasuka baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
PICHA NA GPLkama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA