Habari muhimu_KUHUSU MTU ANAYEHISIWA KUWA NA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/habari-muhimukuhusu-mtu-anayehisiwa.html

Mhudumu wa afya akiwa katika hali ya tahadhari ya Ebola
huko Afrika Magharibi
Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania
Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi
wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na
homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Amesema
sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa
virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini
Benin.Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo
tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari
katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya
watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa
hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha
taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa
Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.
chanzo bbcswahili
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA