Mtu mmoja afa papo hapo baada ya lori kuparamia makazi ya watu na kupinduka jijini Mbeya.
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/mtu-mmoja-afa-papo-hapo-baada-ya-lori.html

Ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa tatu asubuhi imehusisha lori la kampuni ya
kichina inayojenga barabara kuu ya Mbeya – Chunya ambalo namba zake
zimeng’olewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo punde tu baada ya ajali
kutokea, lakini mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni breki za lori hilo kukatika likiwa kwenye mteremko mkali hali
iliyosababisha kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye makazi ya watu.
Wamiliki
wa nyumba ambayo imeparamiwa na lori hilo, Emmanuel John Sangu na mkewe
Monica Sangu wamesema kuwa kitendo cha lori hilo kuparamia nyumba yao
kilihatarisha maisha yao na familia yao na kuwa ingawa wamenusurika
wamepata hasara ya kuvunjiwa ukuta wa uzio wa nyumba yao.
Jeshi
la polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema
kuwa mtu aliyepoteza maisha alikuwa ni dereva wa lori hilo ambaye jina
lake bado halijafahamika.
Chanzo ITV
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA