HUU NI USHAURI WA BURE KUTOKA KWA H-BABA KWENDA KWA DIAMOND NA WEMA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/huu-ni-ushauri-wa-bure-kutoka-kwa-h.html
Msanii
wa muziki na filamu H.Baba ambaye yupo ndani ya ndoa na msanii mwenzake
Flora Mvungi ametoa maoni yake kwa kile kinachooendelea kati ya pande
mbili za kishabiki za Diamond na mpenzi wake Wema.
Kupitia
ukurasa Instagram, H.Baba amesema: Tanzaniteone uyo anawaambia sina
chakusema kuhusu baba yangu na mama yangu ila baba analolakuwaambia Wema
na Naseeb.
Wema
kapewa lawama nyingi ila asilaumiwe kwasababu kuu nyingi tu anaeweza
kumuongoza Wema ni Naseeb au mama Wema na Martin, upande mwingine Wema
na Daimond wanamakosa kwani wanasubiri nini kuowana kama Kweli
wanapendana wangefunga ndoa yaya yote yasingetokea kusaidiana kazini ipo
ata mie huwanapanda na Mama Tanzaniteone kwenye show zangu pia filamu
ya wife nashiriki. ushauri wangu Diamond unaweza kumuongoza Wema vyema
tuu kama mimi ninavyomuongoza Mama Tanzaniteone ninaimani unaweza
kumuongoza vyema zaidi yetu sisi.
Wawili
wakipendana kuingilia penzi ni inshu ila wanapendezana sana chamsingi
wangesaidiana kwenye kazi zaidi kama wema anavyoonekana akitoa #saport
kubwa kwa #NASEEB na naseeb aonyeshe ushirikiano kwenye mov za wema
awepo pia watauza sana kama tunavyouza filamu zetu Mie
namamatanzaniteone Ikitoka leo inaisha fasta.
Pia
amuongoze kwenye kipindi cha WEMA SHOW mnasaidiana kwelii ata maadui
wataogopa #diamond anaweza kumpandisha wema na wema anaweza kumpandisha
#daimond wote mnanguvu sana mnamashabiki sana #owaneni mtulie tuuu kwani
nn mnakosa mbona sisi tupo tunaishi vyema kwa uwezo wa mungu kazi
tunapata mtoto tunamlea vyema hatujalala Njaa kwasababu mwanaume kazini
mwanamke kazini #NDOA raha sana asikudanganye mtu unaheshimika popote
palee kama #Mume wa mtu na #mke wa mtu #Muda ndo huu umriii uwoo
unakwenda fanyeni yenu fasta #leo juu kesho chini #tunawapenda sana
tunawatakia maisha mema yenye Furaha kama sisi apa tunafuraha Muda wote?
Karibuni kwenye ndoa muone rahaaa..
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA