Israel itaharibu njia za chini kwa chini
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/israel-itaharibu-njia-za-chini-kwa-chini.html

Israel inasema kuwa haitaondoka Gaza hadi iharibu njia za chini kwa chini
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin
Netanyahu amesema kuwa Israel imeamua kuyaharibu kabisa mahandaki na
njia za chini ya ardhi zilizojengwa na wapiganaji wa Palestina-Hamas,
katika mipaka yake huko Gaza.
Amesema uharibifu huo utatekelezwa na majeshi ya Israeli kukiwa au kutokuwa na muafaka wa kusitisha mapigano.Netanyahu amesema hayo huku Serikali ya Israel ikishikia kani kuwa kuwa itaendeleza mashambulizi katika eneo la Gaza licha ya shutma za kimataifa kufuatia shambulizi la shule moja ya umoja wa mataifa ambapo takriban watu 15 walipoteza maisha yao.

Mwanamke akiomboleza Gaza
Umoja wa mataifa umesema kuwa ni wazi kwamba ni jeshi la israel ndilo lililorusha kombora hilo katika shule hiyo ambapo zaidi ya raia elfu tatu wa Palestina walikuwa wameomba hifadhi.
Licha ya malalamiko kutoka kote duniani kuhusiana na idadi kubwa ya vifo vya

Njia za chini kwa chini za Hamas ambazo Israeli inalenga kuharibu
Na sasa Israel inajiandaa kwa vita zaidi baada ya kuwaamuru wanajeshi wa akiba kujiunga na jeshi la taifa. Katika ukanda wa ngaza ni kilio na majonzi makubwa...
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA