KESI YA WANABLOGU KUMI YAAHIRISHWA HADI AGOSTI 2014
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/kesi-ya-wanablogu-kumi-yaahirishwa-hadi.html

Kesi hiyo ilianza leo miezi mitatu baada ya tisa kati yao kukamatwa na polisi.
Mmoja wa wanablogu hao alishtakiwa bila kuwepo mahakamani.
Wanakabiliwa na mashitaka ya ugaidi chini ya sheria iliyoshutumiwa ya kupinga ugaidi.
Kesi hii imevutia hisia kubwa nje na ndani ya Ethiopia, hiyo basi hakukuwa na tofauti kubwa ilipoanza hivi leo.
Mahakama hiyo ilijazwa na raia wa Ethiopia, wanahabari hali kadhalika maafisa wa kidiplomasia.
Wote
walioshitakiwa walifika mahakamani. Mawakili walikuwa wamepinga kwa
mapema mashitaka hayo wakisema kuwa hayakuwa na msingi.
Hata
hivyo mahakama ilikataa kuwaachilia kwa dhamana wanablogu hao jinsi
walivyokuwa wakitaka mawakili wao. Wote kumi wameshitakiwa kwa kubuni
kikundi haramu vile vile kushirikiana na makundi ya upinzani yaliyopigwa
marufuku ng’ambo na nchini.
Waendesha mashtaka walisema kuwa washtakiwa hao walipokea ufadhili na mafunzo ya kutengeneza vilipuzi.
Kitendo
hicho cha kuwakamata wanablogu kimesababisha serikali ya Ethiopia
kushutumiwa kimataifa na kutaja kuwa inatumia sheria dhidi ya ugaidi
kukandamiza upinzani na uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.
Katika
mahojiano ya hivi majuzi na BBC waziri mkuu wa Ethiopia alikanusha
madai ya kuwakandamiza wanahabari lakini akasema kuwa serikali
haitawavumilia wanablogu na wanaharakati wanaonekana kushirikiana na
makundi ya kigaidi nchini humo.
Chanzo bbcswahili
kama huja like
ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia
punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu LIKE HAPA