KIKONGWE AJIOMBEA KIFO SABABU YA KUISHI KWA MANYANYASO, HUKU AKIJICHONGEA JENEZA


Mkazi Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia. 
 Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu
anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi. 
 Nimetengeneza kabisa jeneza langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka ili kuepukana na mateso haya. 
Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo. 
Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa masikitiko. Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja. 
Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza.

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu LIKE HAPA


Related

MATUKIO 5177865845733196366

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item