KIJANA ADAIWA KUTAPELI PIKIPIKI AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO NA MAWE KISHA KUCHOMWA MOTO_KAHAMA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/kijana-adaiwa-kutapeli-pikipiki-auawa.html
Wananchi wakitazama eneo la tukio |
Kijana
mmoja aitwaye Daniel John (30) Muha mkulima na mkazi wa Majengo
Kahama ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake
na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kutuhumiwa
kuiba/kutapeli pikipiki.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa sita mchana katika mtaa na kata ya Nyihogo mjini Kahama, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

Gari la Polisi likiondoka eneo la tukio baada ya kuuchukua mwili wa Marehemu |
Taarifa
zinadai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa
alikodisha Pikipiki hiyo zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la
Maegesho ya Daladala za Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya
hiyo.
Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya pikipiki, inadaiwa alimkamata mhutuhumiwa maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi akiwa amemfunga kamba.

Imeelezwa
kuwa baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo
wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza
kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwa
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mara baada ya
mauaji hayo wananchi na mmiliki wa pikipiki walitoweka na pikipiki hiyo
na kwemda nayo kusikojulikana.
Kamanda
Tibishubwa amesema jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kuwabaini
na kuwakamata wahusika wote wa mauaji hayo sambamba na mmiliki wa
pikipiki hiyo.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.
Aidha
ametoa hamasa kwa wananchi kuacha mara moja tabia ya kujichukulia
sheria mkononi kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi na haki za binadamu.
Na malunde1 blog
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA