Kufa kufana: Mfanyakazi wa benki afikishwa mahakamani kwa kuiba pesa za abiria walipotea na Malaysia airline
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/kufa-kufana-mfanyakazi-wa-benki.html

Mwanamke
mmoja mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyopo Kuala Lumpur
Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba pesa kutoka katika
account za abiria na wafanyakazi wa ndege ya Malaysia iliyopotea kwenye
bahari ya hindi.
Pamoja
na kushtakiwa huko mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine 16 kati ya
makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa
huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki
ya HSBC nchini Malaysia kwa kuiba pesa za abiria walipotea na ndege.
Mwendesha
mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba
wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini
kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja
ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia airline.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA