MAJANGA - DEREVA BODABODA MBARONI KWA KUMNG’ATA MWENZAKE MDOMO NA KUONDOKA NAO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/majanga-dereva-bodaboda-mbaroni-kwa.html
DEREVA wa bodaboda, Adinan Adam, mkazi wa Kata ya Olorieni, mkoani Arusha ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumng’ata mdomo Shabani Temba na kuondoka nao.
Akizungumza
kwa uchungu wakati akitoa maelezo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha
Olorieni, Shabani alisema ameshangazwa kujikuta anapigwa kisha kung’atwa
mdomo na kutolewa nyama ya mdomo pasipokuwa na kosa lolote.
Temba
alisema, Alhamisi iliyopita, majira ya saa 12 jioni alifika katika
kijiwe cha vyuma chakavu katika kata ya Olorieni akiwa amechoka kutokana
na mizunguko yake, ndipo alipoona akae juu ya bodaboda iliyokuwa
imeegeshwa kijiweni hapo huku watu wengine wakiwa pembeni yake.
“Nilipokuta pikipiki (bodaboda) hiyo ikiwa imeegeshwa katika kijiwe hicho kutokana na hali yangu ya kuchoka, niliamua kuikalia ndipo ghafla mtuhumiwa alipotokea na kuanza kunishambulia kisha kuning’ata hadi kuondoa nyama yote ya mdomo wangu,”
alisema mlalamikaji huyo.
Mtuhumuiwa ambaye ni dereva wa bodaboda, Adinan Adam(aliyesimama) akiwa Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, mkoani Arusha.
Alisema
baada ya kutendewa tukio hilo, alipiga kelele hali iliyosababisha
wasamaria wema waliokuwa katika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa na
kumfikisha katika kituo cha polisi ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Kwa
upande wake mtumuniwa huyo alipohojiwa sababu ya kutenda kosa hilo
alisema ilikuwa ni hasira za kishetani kwa kuwa alifikiri kitendo cha
mlalamikaji kukaa kwenye bodaboda yake kungesababisha kuibiwa.
Mtuhumiwa
huyo aliomba asamehewe akidai kuwa alifanya tukio hilo kwa sababu ya
hasira ambapo amebaini ni kosa baada ya kutiwa mbaroni na jeshi la
polisi.
Hata
hivyo, baadhi ya wananchi wamelaani kitendo hicho na kudai kuwa
kinaweza kuhusishwa na viashirio vya mazingira ya vitendo vya
kishirikina.
“Kitendo alichofanyiwa Shabani siyo bure kitakuwa na mambo ya kishirikina, inabidi ahangaike kujua undani wake,”
alisema kijana mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Jeshi
la polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
tayari limeshamkamata mtuhumiwa ambaye amefunguliwa jalada la kesi ya
jinai Namba AR/RB/10937/2014 KUJERUHI.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA