MAKUBWA NA MAZITO HAYA: LADY JAYDEE SASA AHAMIA HOTELINI!
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/makubwa-na-mazito-haya-lady-jaydee-sasa.html
Judith Wambura ‘Jide’ akipozi.
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’.
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni
ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa
kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay
jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.
Wiki
iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza
kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini
Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.
Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.
Hata
hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita
lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini
alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.
Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani.
Baadhi
ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner
miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini
hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!
Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo
alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa
muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka
nayo.
Mmoja
wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii huyo
kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo,
kwa kile
alichodai kuwa haieleweki.“Ni kweli Anaconda (Jide) anaishi pale, wewe
nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo,”
alisema mtu huyo.
Juhudi
za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku ikielezwa
kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika
kirahisi katika simu yake ya mkononi.
Imeandikwa na Shakoor Jongo, Gladness Mallya na Chande Abdallah.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA