MAITI YAZIKWA KIMAAJABU DAR ES SALAAM,KICHWA MIGUUNI,SANDA NYEUSI YATUMIKA BADALA YA SANDA NYEUPE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/maiti-yazikwa-kimaajabu-dar-es.html
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kushangaza, wananchi wa Mbezi Msakuzi
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walisusa na kuondoka
makaburini kwa kile kilichodaiwa kuwa maiti ya Michael Kisanto (pichani)
waliyotarajia kuizika iliwekwa ndani ya jeneza kimaajabu.
Tukio
hilo lilitokea hivi karibuni katika Makaburi ya Makamba Msakuzi, Mbezi
jijini Dar es Salaam ambapo wananchi hao waligundua kuwa maiti ya
kijana huyo iliweka ndani ya jeneza kinyume na utaratibu uliozoeleka
yaani kichwa chake kilielekezwa sehemu ya miguu na miguu ilielekezwa
sehemu ya kichwa.
\Kama
hiyo haitoshi, maiti hiyo badala ya kuviringishwa sanda nyeupe,
ilitumika sanda nyeusi kitu kilicholeta tafsiri tofauti miongoni mwa
waombolezaji.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, kabla jeneza lenye mwili
kutumbukizwa kwenye kaburi kulitokea mvutano mkubwa baina ya wanandugu
na waombolezaji.
Imeelezwa
kuwa, waombolezaji hao waliwataka wanandugu wafuate taratibu
zilizozoeleka katika jamii wakati wa kuzika.Hata hivyo, ndugu wa
marehemu hawakuwasikiliza na kudai kwamba walikuwa wanafuata mila na
tamaduni za kabila lao (jina la kabila linahifadhiwa kwa sababu maalum).
Mwili wa marehemu, Michael Krisanto ukishushwa kaburini.
Wanandugu
hao wakaamua kushusha jeneza lenye mwili kaburini na walipoanza kuzika
waombelezaji walikuja juu na kulitoa jeneza kaburini hali iliyosababisha
kutokea kwa vurugu kubwa.
“Vurugu
hizo zilisababisha wanawake waliokuwa makaburini kutimua mbio na
wanaume wakasusa na kuwaacha wanandugu waendelee kumzika ndugu yao,”
alisema shuhuda wa tukio hilo kwa sharti la kutoandikwa jina lake
gazetini.
Habari
zinasema kuwa, kutokana na utata huo, hata mchungaji aliyepaswa
kuendesha ibada ya mazishi aliondoka bila kutoa huduma ya kiroho.
Mmoja
wa wanandugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Victor,
alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo hakuweza kusema chochote badala yake
alikuwa akibubujikwa na machozi.
via>>gpl
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. like hapa