MENINAH:HATUENDANI NA DIAMOND
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/meninahhatuendani-na-diamond.html
STAA wa
muziki wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah’ amefunguka juu ya
tetesi zinazoeneo kuwa na uhusiano wa chinichini na Nasib Abdul
‘Diamond’ kwa kusema kuwa siyo levo yake.
Akichonga
na paparazi wetu, Meninah anayetamba na ngoma ya Pipi ya Kijiti
alikanusha na kusema kuwa, wote ni mastaa lakini wametofautiana kwa
kiasi kikubwa na kwamba hawezi kuwa naye katika mahusiano ya aina
yoyote.
“Kwanza
nilishawahi kukutana naye kwenye shoo tofauti na zote sikuwahi hata
kuzungumza naye chochote, ni staa na mimi staa lakini tunatofautiana
kuwa yeye yupo juu yangu,” alisema Meninah.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA