Mwanamke 'aliyeasi dini' awasili Marekani
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/mwanamke-aliyeasi-dini-awasili-marekani.html

Mumewe Meriam ni raia wa Marekani
Mwanamke wa Sudan aliyetoroka
kutoka nchini humo baada ya kunusurika hukumu ya kifo kwa kosa la ‘kuasi
dini ya kiislamu’,Meriam Yahia Ibrahim Ishag, amewasili Marekani.
Alihukumiwa kunyongwa mapema mwaka huu lakini
baadaye akaachiliwa huru mwezi Juni baada ya ulimwengu mzima kukemea
uamuzi huo uliotolewa na mahakama moja nchini humo.Babake Bi. Ibrahim ni muislamu na hivyo basi inavyoambatana na sheria za kiislamu za Sudan Bi. Meriam pia ni muislamu na hawezi kuasi dini ya kiislamu.
Lakini Meriam amesisitiza kuwa hajawahi kuwa muumini wa dini ya kiislamu kwani alilelewa na mamake ambaye ni Mkiristo.
Kufuatia malalamiko kutoka kote ulimwenguni, aliachiliwa huru mwezi Juni. Bintiye Meriam, Maya, alizaliwa gerezani mwezi Mei. Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, Meriam alizuiliwa kutoka nchini Sudan na familia yake ikalazimika kutafuta hifadhi katika ubalozi wa Marekani uliopo Khartoum.
Bi. Ibrahim aliwasili Philadelphia kwa ndege Alhamisi jioni kutoka Rome, Italia akiwa na mume wake wa kimarekani.
Mumewe Bi Meriam, Daniel Wani, pia ni muumini wa kikiristo na pia ni mzaliwa wa Sudan kusini lakini ana uraia wa kimerakani.

Meriam aliponea kifo baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wa kumnyonga kwa kuasi dini
Rosa Parks alisifika na kutazamwa kuwa ushujaa wa harakati za haki za kiraia nchini Marekani alipokataa kuondokea mwanamme mzungu kitini wakiwa ndani ya gari huko Alabama.
Hatimaye Nutter alimkabidhi Meriam mfano wa ‘kengele ya uhuru,’ ishara ya uhuru wa Marekani. Aidha, kwa mujibu wa msemaji wa Vertican, Bi Meriam akiwa Rome alikutana na papa ‘aliyemshukuru kwa kuwa imara katika Imani yake.”
Safari ya Bi Meriam ilifikia kikomo New Hampshire kwani alikuwa anasubiriwa kwa hamu na ghamu na jamaa na wafuasi wake katika uwanja wa ndege.

Alipoondoka Sudan alipitia Italy ambako alikutana na Papa Francis
Aidha mwanahabari wetu alituarifu kuwa mume wa Bi Meriam alitoa hotuba fupi na kushukuru serikali ya Marekani na maseneta wa New Hampshire kwa kumpigania na kwa kufanya mipango ya kumpa mke wake hifadhi. Pia alishukuru watu wa Sudan kwa usaidizi wao.
Familia ya Meriam inakusudia kuishi New Hampshire kwani jamaa wa mume wake wako huko.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA