NEWZ :- PAPA FRANCIS ATABIRI KIFO CHAKE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/newz-papa-francis-atabiri-kifo-chake.html

Akiongea
na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akirejea Vatican kutoka
ziarani nchini Korea Kusini, Papa Francis amesema kuwa suala la
kuendelea kuishi ni neema ya Mungu na kwamba atafariki baada ya miaka
miwili au mitatatu.
“Suala
hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari
kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu
hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa
nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba.” Amesema Papa Francis.
Ingawa
Papa Francis mwenye umri wa miaka 77 hajawahi kuzungumza hadharani
kuhusu suala la afya yake, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka
Vatican vimeeleza kuwa amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuhusu
siku zake chache zilizosailia dunia.
Wachambuzi wa masuala ya kiimani wameeleza kuwa huenda Papa Francis ana tatizo la kiafya ambalo hakuliweka wazi.
Chanzo: Mwananchi