SAGNA ATOA YA MOYONI WATU WALIOMSHAWISHI KUJIUNGA NA MAN CITY
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/sagna-atoa-ya-moyoni-watu.html

Beki
wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Bacary Sagna, hatimae amefichua siri
nzito iliyokuwa imejificha moyoni mwake, baada ya kuikacha klabu ya
Arsenal na kukubali kujiunga na Man City.
Sagna,
amelazimika kufichua siri hiyo ikiwa ni siku chache baada ya
kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Man City ambayo aliwahi
kuikana kwa kusema haikuwa kwenye mawazo yake mara tu, alipokataa
kusaini mkataba mpya na Arsenal.
Beki
huyo ambaye ameondoka kaskazini mwa jijini London akiwa sehemu ya
kikosi kilichorejesha heshima kwa kutwaa ubingwa wa kombe la FA msimu
uliopita, amesema sababu kubwa ya kujiunga na mabingwa hao wa nchini
Uingereza ni ushawishi alioupata kutoka kwa Samir Nasri pamoja na Gael
Clichy.
Amesema
kwa kipindi kirefu tangu wachezjai hao wawili walipoihama Arsenal,
amekuwa akiwasiliana nao katika masuala yanayohusu maisha pamoja na
urafiki uliopo baina yao, lakini miezi kadhaa iliyopita mazungumzo yao
yalihamia kwenye ushawishi wa kumtaka ajiunge nao kwenye klabu ya Man
city.

“Nilizungumza
nao [Nasri na Clichy], mara nyingi zaidi na walinihakikishia uwezekano
wa kusajiliwa kwenye klabu hii, na waliniambia mazingira yaliopo hapa,
hivyo nilifanya maamuzi ya kujiunga na Man city.”
"Walijua
mkataba wangu na Arsenal unamalizika mwishoni mwa msimu uliopita, hivyo
waliitumia nafasi hiyo kunishawishi kwa usiku na mchana”.
"Wachezaji
walio hapa wanajitahidui kufanya kazi kwa bidii ili wakamilishe malengo
ya kutwaa vikombe kadhaa kila msimu, hivyo nimeona na mimi niwe sehemu
yao.'
"Nimeitumikia
Arsenal kwa kipindi cha miaka saba iliyopita na mengi mazuri yalikuwepo
kwenye klabu hiyo mpaka kufikia hatua ya kurejesha heshima ya kutwaa
ubingwa wa FA msimu uliopita, na sasa ni wakati mzuri kwangu kuanza
mwanzo nikiwa na klabu mpya”.
"Kwangu,
Man City ni klabu kubwa, na sina budi kuitumikia kwa moyo wangu wote
kutokana na malengo niliyoyakuta hapa.” Amesema Sagna mwenye umri wa
miaka 31
Bacary
Sagna ameondoka Arsenal huku akiacha kumbukumbu ya kucheza michezo 213
na kufunga mabao manne tangu mwaka 2007 aliposajiliwa na klabu hiyo ya
Emitares Stadium, akitokea nyumbani kwao Ufaransa kwenye klabu ya
Auxerre.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA