UNYAMA: NJEMBA YAMNYWESHA VIROBA MTOTO KISHA KUMBAKA HUKO IRINGA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/unyama-njemba-yamnywesha-viroba-mtoto.html
Watu
wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma
mbalimbali ikiwepo ya mtu mmoja kushikiliwa na jeshi la polisi kwa
tuhuma ya kumnywesha pombe mtoto wa miaka 14 kisha kumbaka.
Kamanda
wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amemtaja mtuhumiwa
kuwa ni Sepelwa Mnyambala umri miaka 25 mkazi wa eneo la kihesa Sokoni
Manispaa ya Iringa anashikiliwa kwa tuhuma ya kumnywesha mtoto huyo
pombe aina ya kiloba kisha kumfanyia unyama huo.
Ameongeza kuwa mtoto huyo ni mkazi wa eneo la Kihesa Manispaa ya Iringa.
Hali hiyo iliyosababishia maumivu makali mtoto huyo huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni tamaa ya mapenzi.
Katika
tukio la pili Kamanda Mungi amesema Mohamed Mfilinge umri miaka 20
mkazi wa Kijiji cha Dinginayo wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa amekamatwa
akiwa na pikipiki aina ya Shineray mali ya wizi akiwa katika harakati
za kuiuza chanzo kikiwa ni tamaa ya mali.
Aidha
amesema jeshi la polisi linawatafuta mtu/watu wasiofamika kwa tuhuma ya
kuiba pikipiki yenye namba za usajili T.645 CNP aina ya Sunlg yenye
thamani ya shilingi 1,700,000 mali ya Modestus Ngusi umri miaka 31 mkazi
wa eneo la Makorongoni Manispaa ya Iringa.
Hata
hivyo Kamanda Mungi amesema katika maeneo ya Mivinjeni Manispaa ya
Iringa nyumba ya Merina Msigala umri miaka 25 imeungua moto baada ya
mtoto wa mpangaji kuchezea kiberiti na kuwasha godoro na ikapelekea
nyaya za umeme kushika moto huo ambapo hasara yake ni shilingi milioni
nne.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA