SERIKALI IMELIONYA GAZETI LA SANI KWA KUCHAPISHA HABARI NA PICHA ZISIZOKUWA ZA KWELI NA UZUSHI TU, ZAZUA HOFU KWA WANANCHI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/serikali-imelionya-gazeti-la-sani-kwa.html
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Assah Mwambene (kulia) akiwaonyesha waandishi wa
habari gazeti la Sani leo mjini Dar es Salaam lililochapisha habari ya
upotoshaji inayoweza kujenga hofu kwa wananchi. es Salaam.Kushoto ni
Afisa Habari anayeshughulika na Usajili wa magazeti Jovina Bujulu.Picha na MAELEZO
Na JOVINA BUJULU
SERIKALI imelionya gazeti la SANI kwa kuchapisha habari na picha zisizokuwa za kweli na kuzua hofu kwa wananchi.
Hatua
hiyo inafuatia na gazeti hilo kuchapisha habari zilizokuwa na kichwa
kisemacho EBOLA YATUA na kuonyesha picha za maiti bila kueleza kuwa sio
za tukio lililotokea nchini.
Onyo
hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Assah Mwambene wakati akiongea na waandishi wa habari.“Sio vizuri na kuleta mizaha katika habari makini na zinazogusa maisha ya wananchi kama ugonjwa wa EBOLA kwa unasababisha hofu miongoni mwa jamii” amesema Mwambene.
Amesema kuwa hadi hivi sasa hakuna mgonjwa yoyote aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hapa nchini na wala haujafika.
Hata
hivyo Mwambene ameongeza kuwa pamoja na kutokuwa na mgonjwa yoyote hapa
nchini, Serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na
ugonjwa huo endapo utaripotiwa kuingia nchini.
Ametaja
hatua hizo ni Kutenga vituo maalum vya kuwapima wagonjwa watakaohisiwa
kuwa na ugonjwa huo katika viwanja vya ndege na sehemu zote za kuingilia
nchini.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA