SIWEZI KUJADILI UPUUZI HUU' ASEMA RAIS KIKWETE KUHUSU TETESI KUWA ALIMUOKOA RIDHIWANI BAADA YA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA!
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/siwezi-kujadili-upuuzi-huu-asema-rais.html

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amesema kuwa ni mkusanyiko wa upuuzi mtupu madai kuwa yeye Rais
alishiriki kumwokoa mtoto wake, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete
ambaye alikuwa amekamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa Urais ni taasisi kubwa sana nchini na hivyo
yeye akiwa Rais hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mtaani,
kama ambavyo wanataka baadhi ya watu wanamsukuma ili ashiriki katika
maneno hayo ya mitaani.
This
is nonsense; ni mkusanyiko wa upuuzi. Sina muda wala siwezi kupoteza
nguvu yangu kujadili upuuzi na ujinga wa namna hiyo, amesema Rais
Kikwete usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipozungumza na
Watanzania wanaoishi katika Marekanikwenye Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C.
Rais
Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani
alitoa majibu hayo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu madai yaliyotolewa
Julai Mosi, mwaka juzi, 2012 na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA,
Wilbroad Slaa, madai hayo yamempeleka mahakamani.
Amesema
Rais Kikwete: “Hatuwezi sisi kujiingiza katika shughuli ya kupoteza
muda kwa kushiriki upuuzi na ujinga. Haya ni maneno ya kipuuzi
yanayosemwa na watu ambao kazi yao usiku na mchana ni kuota jinsi ya
kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali
ya maisha ya Watanzania.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Urais ni taasisi kubwa sana. Rais wa nchi yetu hawezi
kujiingiza katika ubishani na watu wa mitaani. Kwanza huyo Ridhiwani
amemfikisha Slaa kortini na mpaka leo hata kesi yenyewe haijatajwa.”
Kuhusu
swali jingine aliloulizwa kuhusu suala hilo, kuwa Rais Kikwete alitia
saini mikataba 12 na uongozi wa Jamhuri ya Watu wa China kama sehemu ya
masharti ya kuachiwa kwa Ridhiwani, Rais Kikwete amesema: “Naipenda nchi
yangu kiasi cha kwamba siwezi kufikiria hata kuiweka rehani.
Haya
ni maneno ya kipuuzi tu, yenye kutafuta kututoa kwenye ajenda zetu
nzuri. Hatuna muda nayo, sisi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mambo ya
maana ya kuleta mabadikio katika ustawi wa Watanzania.”
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es Salaam.
04, Agosti, 2014
kama huja like
ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia
punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu LIKE HAPA