TAARIFA KAMILI KUHUSU BINTI ALIYEANGUKIWA JIWE KUBWA NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO HUKO KAHAMA AKICHIMBA KOKOTO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/taarifa-kamili-kuhusu-binti.html
![]() |
Wananchi wakiangalia jiwe lililomwangukia na kumfunika Marehemu Lucia Bahati![]() Afisa mtendaji wa Kijiji cha Shunu Benjamin Makelo akielezea tukio hilo lilivyokuwa. |
Mkazi
wa kijiji cha Shunu kata ya Nyahanga Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,
Lucia Bahati (25) amefariki dunia papo hapo baada ya kuangukiwa na jiwe
katika eneo lililokuwa likitumika kutengeneza kokoto kijijini humo.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa nne asubuhi wakati Lucia na wenzake
wakichimba kokoto katika eneo hilo lililopo katika kitongoji cha
Ikorongo ambalo liliwekwa mashine za kutengeneza kokoto wakati wa ujenzi
wa Barabara za lami wilayani Kahama.
Kwa mujibu wa Angela Alex ambaye walikuwa wakichimba kokoto katika eneo
hilo na Marehemu, jiwe hilo lilikuwa limekaa vibaya na kwamba walikuwa
wakifanya kazi kwa tahadhari kabla ya kumuangukia mwenzake.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Shunu Benjamin Makelo, amesema baada ya
tukio hilo, wananchi walifika kusaidia kusogeza jiwe hilo na kuutoa
mwili wa Lucia ambaye ni mzaliwa wa Ilogi wilayani humo, akiwa tayari
ameshafariki.
Makelo
amesema awali baada ya kupata taarifa za tukio hilo alipiga simu polisi
ambao baadae walifika na kuuchukua mwili wa marehemu ambao sasa
umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya
ya Kahama.
Kufuatia
tukio hilo, Afisa mtendaji wa kata ya Nyahanga William Upamba
amesitisha shughuli za uchimbaji wa kokoto katika eneo hilo ambalo ni
hatari kwa maisha ya watu, na ametoa siku 10 kwa wenye kokoto zao
kuhakikisha wameziondoa.
Chanzo Malunde1 blog
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA