WACHEZAJI 10 BORA BARA LA ULAYA WATAJWA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/wachezaji-10-bora-bara-la-ulaya-watajwa.html
Robben ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya
Kipa
wa Ujerumani na Bayern Munich Manuel Neuer Mshambulizi wa Uholanzi
Arjen Robben wamejiunga na mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni miongoni mwa wachezaji wanaowania
taji la mchezaji bora barani Ulaya.
Watatu hao walichaguliwa na waandishi wa habari za michezo kufuatia utendakazi wao uwanjani katika msimu wa mwaka wa 2013-2014.

Mshindi atatangazwa rasmi tarehe 28 mwezi huu.
Muller ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya
Nuer alikuwa ngao ya mabingwa wapya wa dunia Ujerumani huku Robben akitikisa wavu mara 21 .
Kwa
upande wake mchezaji bora duniani mwaka huu Christiano Ronaldo alifunga
mabao 17 msimu huu na kuiongoza Real Madrid Kutwaa taji la mabingwa
barani Ulaya.
Mshindi atatuzwa katika hafla ya kutangaza droo ya mwaka huu ya kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya huko Monaco.

Costa ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya
Wachezaji kumi waliteuliwa kulingana na wingi wa pointi waliozojizolea .
Wengine
katika Orodha hiyo ni Thomas Muller (Bayern Munich, ) 39 ; Philipp Lahm
(Bayern Munich, ) 24, Lionel Messi (Barcelona, Argentina) 24; James
Rodriguez (Monaco/Real Madrid, Colombia) 16; Luis Suarez
(Liverpool/Barcelona, Uruguay) 13; Angel Di Maria (Real Madrid,
Argentina) 12; Diego Costa (Atletico Madrid/Chelsea, Uhispania ) 8.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA