WATU NANE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWL.NYERERE WAKIINGIA NCHINI KWA PASPOTI BANDIA ZA MATAIFA TOFAUTI YA ULAYA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/watu-nane-wakamatwa-uwanja-wa-ndege-wa.html
Idara
ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati
wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere,
wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya.
Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014
majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la
Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa
Raia wa Sweden na Belgium.
Maofisa
Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia
ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu
kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
kukamatwa
kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji
haramu nchini ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele.
akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu
Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji
wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria
na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa.
"Idara
ya Uhamiaji, iko macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi
ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe
Raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na
Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini" .
Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea
kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri
kurudishwa walikotoka. Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa
baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini
isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na
baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.Majina
ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina
halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye
mabano ni kama ifuatavyo;
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA