MJANE ALIPULIWA KWA MOTO WA PETROLI NA KUFARIKI DUNIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/mjane-alipuliwa-kwa-moto-wa-petroli-na.html
MAMA
mmoja mjane, Mwajuma Hamisi Lissu (42) ameteketea kwa moto baada ya
nyumba aliyokuwa amelala eneo la Kibamba Hondogo A maarufu Miti Mirefu
jijini Dar es Salaam, kulipuliwa kwa petroli usiku wa Agosti 24, mwaka
huu.
Tukio
hilo la kusikitisha inadaiwa linahusishwa na ugomvi baada ya mama
huyo kuachana na ulokole na kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya
Kiislamu.Akisimulia mazingira ya tukio hilo, mtoto wa pili wa mama huyo
ambaye hivi sasa ni marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charity
Jikole alikuwa na haya ya kusema:
“Mama
amelipuliwa na petroli. Baada ya moto huo kulipuka chumbani tulikuta
nyavu za kwenye dirisha la chumba alicholala zimekatwa, tunaamini
mlipuaji ndiye aliyekata nyavu hizo na kupitishia petroli.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV1boIpbPq6ceh91z-2t99Gf-uLKPTJT8aZxJaESaLflFAwRfZQ_GGvCCRrEQLCsMax5m0dWUI_n9yRR-8od1lFEFTDFgPhXHKnKySoxHBrvoiwEzwDQw9q9AaGF9NLDf8XoPE5pkHRPJ9/s1600/2+(24).jpg)
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV1boIpbPq6ceh91z-2t99Gf-uLKPTJT8aZxJaESaLflFAwRfZQ_GGvCCRrEQLCsMax5m0dWUI_n9yRR-8od1lFEFTDFgPhXHKnKySoxHBrvoiwEzwDQw9q9AaGF9NLDf8XoPE5pkHRPJ9/s1600/2+(24).jpg)
“Mkasa
huu unatokana na ukweli kuwa mama yangu awali alikuwa Muislamu lakini
kutokana na matatizo yake ya kiafya alishauriwa na baadhi ya watu
kujiunga na maombi katika makanisa ya kilokole ili awe anaombewa tatizo
la presha.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.
“Mama alikuwa ni mjane mwenye watoto watatu na baada ya kujiunga na walokole amekuwa akisali katika makanisa manne tofauti.
“Sisi kama familia tunawatuhumu walokole kwa sababu hata baada ya moto huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
“Sisi kama familia tunawatuhumu walokole kwa sababu hata baada ya moto huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
“Kwa kweli tulishangazwa na kitendo hicho na kuwaona ni watu wabaya sana kwetu.”
Hata
hivyo, mtoto huyo alisema kifo cha mama yake kimekuja siku moja baada
ya kufanyiwa sherehe ya kutoka katika dini ya kilokole na kurudi kwenye
Uislamu.
Mchungaji
aliyetajwa kwa jina la George Said ambaye anawaongoza walokole wa eneo
hilo, alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kusikia tuhuma hizo.
“Hata mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema mchungaji huyo.
“Hata mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema mchungaji huyo.