MKE WA BEST MAN WA BWANA HARUSI AJIFUNGUA WAKATI WA SHEREHE,TUKIO LIKO HAPA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/mke-wa-best-man-wa-bwana-harusi.html
msaada wa mtandao wa Daily Mail
MWANAMKE
ambaye alitakiwa kuwa matroni na kisha kumkatalia rafiki yake kwa kuwa
alikuwa mjamzito na aliogopa kumharibia shughuli yake, amejikuta
akikimbilia katika gari kwa ajili ya kujifungua muda mfupi tu baada ya
kuingia katika sherehe za rafiki yake.Alisema awali kwamba alikataa kuwa
matroni kwa kuhofia sit u kuvuruga shughuli ya jamaa yake pia alikuwa
anaona ataharibu picha za harusi.Lakini kwa kitendo chake hicho alikuwa
ndani ya harusi kw akujinafasi sana.
Imeelezwa
katika mtandao kwamba akiwa kama mgeni katika sherehe hiyo mwanadada
huyo alijikuta akuitoka kasiu katika sherehe za rafiki yake
aliyetambulika kwa jina la Amanda Vasey baada ya kuvunja chupa wakati
akiingia kushiriki sherehe hiyo.Vasey, 37, anasema kwamba
moja ya picha znuri kabisa anayioipenda ni ya yeye, mumewe Steven Vasey,
35, na marafiki zao hao Gareth na Amanda Hutchinson wakiwa hospitalini
na binti wa marafiki zao baada ya kujifungua kwa dharura katika gari.
Ndoa ya Vasey, ilifanyika Jumamosi katika hoteli ya King iliyopo Darlington.
Bibi harusi Amanda Vasey akielekea wodini kumsalimia shoga yake.
“nilikuwa
ndio namaliza kujivika nguo wakati Gareth, ambaye ndiye msimamizi wa
mume wangu alipoingia akikimbia na kusema kwamba Amanda ameanza kazi ya
kujifungua.
“kwanza
sikuamini nilizania anafanya mzaha kwani alikuwa na kitetemo cha hotuba
katika harusi kiasi alikuwa akitania kwamba atamwaga maji kwa
kuhangaika. Sasa aliposema mkewe amevunja chupa nilidhani anatafuta njia
ya kukwepa kutoa hotuba ya harusi.
“Baadae nikaona hatanii ndipo mama yangu na wasaidizi wengine wakatoka mbuio kwenda kutoa msaada.
“
walilazimika kuchukua shuka kubw akutoka katika hoteli ili kumpatia
faragha ndani ya gari ambako ndilko alikuwakiwa akijifungulia.”
Anasema
kulikuwa na hamaniko kubwa kiasi ya kwamba kila mtu alikuwa anataka
kumuona na hivyo wakalazimika kuifunika gari ili amalize shughuli yake
kwanza.
“Bahati nzuri hapakuwepo na shida na hivyoi motto aliingia duniani salama.” Alisema bi harusi.
Hutchinson
alijifungua motto aliyekuwa na paundi saba na aonzi 9 na akakambizwa
hospitalini akifuatiwa na mumewe Gareth, 28, hivyo kumwacha bwana
harusi bila msimamizi.
est man na maharusi wakifurahia habari njema za kujiungua salama kwa matroni kabla ya kuelekea hospitali.
Vasey
amesema: ‘Amanda ni mmoja wa marafiki zangu wakubwa na nilitaka awe
sehemu ya waliokaribu nami siku ya harusi yangu, lakini alipogundua
kwamba yeye ni mjamzito alikataa kuwa matroni.
“Alikuwa
ameshajaribu nguo za matroni na kila kitu lakini baadae akasema
ataharibu picha za harusi akakataa kushiriki. NBikamwambia usijali
lakini akasema hataki kuharibu picha .
“ni
kitu cha kuchekesha kidogo, lakini hakutaka hata kushiriki vikao kwa
sababu yeye ni mjamzito, hakutaka kuwa katika hartusi lakini mwishoni
mwa siku kila kitu kilimgusa yeye.”
Bi
Harusi Amanda Vasey na shoga yake Amanda Hutchinson aliyembeba mtoto
wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja Alfie., huku mume wake Gareth
Hutchinson (mpambe wa bwana harusi) akiwa amembeba binti ya mchanga
aliyezaliwa muda mfupi kabla ya ndoa ya bwana harusi Steven Vasey
(aliyesimama).
Rafiki huyo aliomba msamaha mfululizo wakati bi harusi alipoenda kumtembelea baada ya kumaliza hafla ambayo haikucheleweshwa.
Vasey
alisendelea kusema: “alikuwa anaomba msamaha muda wote kwamba
ameniharibia siku yangu. Kumbe sivyo kabisa ameleta Baraka kubwa katika
siku nyangu ya harusi na sasa nitamkumbuka motto muda wote.
“
Nilipoenda kumtembelea tulipoonana nililia, wote tulilia, ilikuwa siku
yangu kubwa. Ninaolewa na Steven na rafiki yangu anamkaribisha motto
duniani.’
Mtoto wa Hutchinson hajapewa jina lakini wanakusudia kumpa jina la Amanda .