MARIO BALOTTELI BAADA YA KUTUA LIVERPOOL, SASA KUNUNUA NYUMBA MATATA KWA PAUNDI MILIONI 4.7
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/picha-tazama-geto-analo-miliki-balotelli.html

Mchezaji huyo wa Liverpool aliyenunuliwa kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16, amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya mji, - eneo la Helsby, Cheshire - na kufanya ndio "keja".
Na
kama picha hizi pamoja na habari ambazo zimeandikwa na magazeti na
tovuti kadhaa nchini Uingereza ni za kuaminika, basi inaonekana
Balotelli ameonesha 'staili' yake kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani
yake ni pauni milioni 4.7.
Nyumba
hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja na kila kitu ambacho mchezaji soka ,
Kijana, milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama bwawa la kuogelea,
sauna, chumba cha kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya kutua helikopta, uwanja wa mpira.. Na vingine 'vidogovidogo'.




