Majambazi
watano waliokipata cha moto katika Majibizano ya risasi na Jeshi la
Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakiwa na siraha za kivita
wakisubiri kuteka magari Alfajiri ya Septemba 03,2014 wakiwa chumba cha
kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Kasulu.
JESHI
la polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya
SMG, mabomu matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu
watano wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za
majibizano baina majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa
polisi mkoa kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira
ya saa 11:45 alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya
Kasulu – Kibondo eneo la pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.
Kwa
mujibu wa kamanda Ibrahim alisema askari polisi wakiwa katika doria
walipata taarifa za majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakitaka
kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kuteka magari ya
wasafiri yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo.
Alisema
kufuatia taarifa hiyo askari polisi walijipanga na kuweka mtego katika
eneo lililokusudiwa kufanyika uhalifu huo ambapo baada ya muda watu hao
walifika eneo la tukio ili kukamilisha azma yao ambapo askari
waliwafuata ndipo walipoanza majibizano ya risasi na askari polisi.
Katika
tukio hilo askari walifanikiwa kuwauwa majambazi wote watano ambapo
katika eneo la tukio hilo walikuta mabomu matatu, silaha mbili za
kivita aina ya SMG No. 691220 pamoja na AK 47 no. UA40501997 magazini
tatu zenye risasi 64 sambamba na mikate na juice aina ya Zaam Zam orange
kutoka katika kampuni ya Monas Beverages.
Kamanda
alisema miili ya majambazi hao ipo katika hospitali ya wilaya ya Kasulu
ambapo majina yao hayajatambulika huku askari polisi waliokuwa katika
tukio hilo wakiwa wamesalimika na hakuna aliyejeruhiwa ambapo msako
unaendelea katika maeneo yote ili kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani
Kigoma.