MWALIMU WA KIKE AUMBUKA VIBAYA SIKU YA HARUSI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/mwalimu-wa-kike-aumbuka-vibaya-siku-ya.html
MWALIMU MMOJA WA SHULE YA MSINGI MAKURUMLA ILIYOPO MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM, MARIA SAMUEL HOZA, AMEJIKUTA AKIAIBIKA VIBAYA BAADA YA MUMEWE, BRYTON MUHANJE KUMKUTA AKIWA KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUFUNGA NDOA NYINGINE KWENYE KANISA KATOLIKI LA KIGOGO LUHANGA, JUMAMOSI ILIYOPITA.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Makurumla, Maria Samuel Hoza akiwa katika harakati za kufunga ndoa yake ya pili.
Gazeti
hili lilimshuhudia Muhanje, akiingia kanisani na kwenda moja kwa moja
mbele ya altare na kumzuia Padri Richard, ambaye alikuwa amemaliza
kufungisha ndoa ya kwanza, asifanye hivyo kwa maharusi wanaofuata kwa
vile ni batili.
Chanzo chetu makini cha habari kililidokeza gazeti hili juu ya kuwepo kwa mpango wa mwanamke ambaye yupo katika ndoa, kutaka kuolewa tena na mtu mwingine bila mumewe kujua. Kufuatia ‘tip’ hiyo, kikosi kabambe cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilifanikiwa kupata namba ya mwanaume huyo na kufanya naye mawasiliano ili kujua ukweli wa madai hayo.
Mume wa Maria Samuel Hoza, Bryton Muhanje akitoa pingamizi la ndoa ndani ya Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga.
Muhanje alikiri kupata tetesi hizo, lakini alikuwa akihaha kujua sehemu itakakofanyika harusi hiyo
na kwamba timu ya vijana wake ilijipanga kuhakikisha anafahamu eneo
hilo.Baadaye aliwaeleza OFM kuwa alikuwa alisikia ndoa hiyo ingefungwa
Magomeni, hivyo alikodi pikipiki sita zilizofanya doria katika makanisa yote yaliyopo eneo hilo ili kujua mkewe alikuwa kanisa gani.
Pamoja na hivyo, mwanaume huyo pia
alikwenda hadi shule anayofundisha mwalimu huyo na kwa kuwa hawamfahamu,
alijitambulisha kama ndugu yake na kwamba alikuwa anaomba kujua kanisa
ambalo (mkewe) atafunga ndoa, kwani ameelezwa kuwa lipo Magomeni lakini
hakuelewa ni lipi.
“Wanafunzi
wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga,
ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo,
nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye
harusi hiyo,” alisema.
Padri Richard akitoka nje ya kanisa hilo mara baada ya pingamizi la harusi kutokea.
OFM
ikiwa tayari kwa kunasa tukio hilo, walikuwa wameshatinga kanisani hapo
mapema na kushuhudia maharusi watatu tofauti wakijiandaa kufunga ndoa,
wakiwemo Maria na mwenzake.
Ratiba ilionyesha kwamba ndoa ya
wawili hao ilikuwa ya pili, hivyo mara tu zamu yao ilipofika na Padri
Richard kuanza kutoa risala ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia, wote
walionekana kuwa na bashasha ya siku hiyo muhimu ya kuungana.
Ghafla bila kutarajia, wakati
wasaidizi wa padri wakimletea kibakuli chenye pete ya ndoa, Muhanje
alijitokeza na kumuomba mchunga kondoo huyo kusitisha zoezi hilo kwa
vile anayetaka kufunga ndoa, ni mke wake halali.
Makamanda wa Polisi wakiwa nje ya kanisa tayari ili kutuliza ugomvi.
Akiwa
amepigwa na butwaa, padri huyo alilazimkika kwanza kumuuliza bibi
harusi kama anamtambua mtu aliyesimama mbele yake, lakini akiwa mkavu
alikataa akidai hajawahi kumuona maishani mwake.
Mume akiwa ameongozana na mpambe
wake aliyesimamia ndoa yake, alimuomba padri atoe vielelezo kuthibitisha
ukweli huo na baada ya kupewa nafasi hiyo,
alionesha picha mbalimbali za siku ya harusi yao, nakala ya cheti cha
ndoa na akaomba pia aruhusiwe atoe kompyuta yake mpakato ili achezeshe
video ya siku hiyo ya Oktoba 29, 2009 alipofunga naye ndoa katika Kanisa
la KKT Kimara Korogwe, Dar.
Kwa ushahidi huo, padri huyo
alikubaliana naye na kusimamisha zoezi hilo na kuwataka kuongozana
kwenda ofisini kwa mazungumzo zaidi. Baada ya mazungumzo marefu ofisini,
padri huyo alikubaliana na hoja za mume na hivyo kusitisha zoezi hilo, akidai mwanamke huyo hawezi kuolewa kwa mara ya pili.
Ilifahamika
baadaye kuwa Maria, ambaye amezaa mtoto mmoja na Muhanje, alitumia jina
la Neema Stanley Hoza katika kusudio lake la kufunga ndoa ya pili.
Baadhi ya wapambe na wanandugu wakirudi makwao mara baada ya ndoa kubatilishwa.
Hata hivyo, wakati kukiwa na sintofahamu ya tukio hilo kanisani, ghafla kikosi cha askari polisi wakiwa katika ‘difenda’
kilitia timu kuhakikisha usalama unakuwepo.Askari hao walisema walipewa
taarifa za kuwepo kwa tukio ambalo lingeweza kuhatarisha amani na ili
kuhakikisha jambo hilo linatokea, waliondoka na maharusi wa pili baada
ya taratibu za Baada ya tukio hilo, Muhanje alisema alimuoa mkewe mwaka
huo, baada ya kuwa ameishi naye kinyumba kuanzia mwaka 2005.“Baada ya
kukaa naye kwa miaka minne, tukaamua kufunga ndoa mwaka huo wa 2009 na baada ya hapo, yeye akaenda kufanya kazi ya ualimu Lushoto katika Shule ya Shambalai.
Picha ya ushahidi ikionesha ndoa ya halali kati ya Bw. Bryton Muhanje na Mwl. Maria Samuel Hoza.
“Mwanzo
tulikuwa na maisha mazuri tu na katika kipindi hicho, nilijitahidi
kumfanyia utaratibu wa uhamisho ili aje Dar na kufanikiwa kumleta mwaka 2012
na alipangiwa Shule ya Makurumla.“Baadaye kidogo hali yangu kifedha
ikayumba, ndipo matatizo yalipoanza kwani kitendo cha kutegemea hela za
mshahara wake katika maisha kikamshinda, akaanza kutafuta visa
mbalimbali ili mradi mimi nimpige apate sababu ya kuondoka.
“Alifanya vituko vingi sana, wakati
mwingine alifunga mlango na kuondoka na funguo na kwenda kwa dada yake
na kulala huko huko, wakati mwingine aliamua tu kuvunja vitu bila kujali
hadi mwaka jana mwezi wa nne alipoondoka moja kwa moja kwenda
kusikojulikana.“Siku chache zilizopita ndipo nilipopata habari kwamba
ana mpango wa kuolewa, ndipo nikaanza kufuatilia ili nijue.
“Nilipokuwa pale kanisani wakati wa kuzuia ndoa, yule mwanaume aliyetaka kumuona mke wangu, alinitishia kuwa atanikomesha, nimeenda polisi kuripoti maana siwezi kujua atafanya nini na nimefungua jalada lenye namba MAG/RB/8452/2014 KUTISHIWA KUUA KWA MANENO.”