JOTI NA LULU MMMH, LULU AACHA MANIDO NJE, JOTI AWAPA KICHWA MASHOGA KWA VAZI LAKE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/joti-na-lulu-mmmh-lulu-aacha-manido-nje.html
Mastaa
wawili Bongo waliokuwa watangazaji wa Shindano la Kuibua Vipaji vya
Kuigiza, Tanzania Movie Talents (TMT), Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Lucas
Mhuvile ‘Joti’ wamezua balaa na kuwaacha hoi mashabiki waliohudhuria
fainali za shindano hilo kufuatia aina ya viwalo walivyokuwa
wamepigilia.
Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi.
Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akitumbuiza jukwaani ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
‘Joti’ akizidi kuwaonyesha vimbwanga vya 'kikomedi' watazamaji waliohudhuria fainali za TMT ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
![](http://api.ning.com/files/bdG71GPfFwHB3TMvXZO-d*HyODk1TbRYRPL8YSuBsvL4JBB4TQi4pbF8Z4sFiSCo6rrRY4fq2LkpgJFSHE2LXS7TlOL0l3Yk/utatalulu.jpg)
Mpango
mzima ulijiri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, wikiendi iliyopita
ambapo katika kuonesha ubunifu, mchekeshaji Joti, alitupia vazi la jinsi
zote ambalo upande mmoja lilionekana ni sketi ya kike na mwingine
suruali ya kiume.
Kama
hiyo haitoshi, mwili wake aliugawa katika nafsi hizo mbili kwani licha
ya sketi, pia mguu wake wa kushoto alivaa kiatu cha kike, kama ambavyo
kichwani kwake, alisuka nywele upande mmoja kama mdada.Kitendo hicho
kilionekana kama kuwapa bichwa wanaume wenye kufanya mapenzi ya jinsia
moja, kwani waliona ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kuvaa mavazi ya
kike.
![](http://api.ning.com/files/bdG71GPfFwEB96jOiKxkv*FHnVqzTfD67C4YHwiNs*8GqlMhl62AlmA6HhA30kUYuGHshTTKtvHyuK3vBQhfIfixUJ6ChBIV/Jotibwabwa.jpg)
Kwa
upande wake, Lulu alivaa kivazi kilichoonesha sehemu kubwa ya mwili
wake, kikiwa kimeziba matiti kwa mbali na kusababisha wanaume wakware
kutokwa na udenda.
Katika fainali hizo za kumsaka mwenye kipaji cha kuigiza ukumbini hapo, mshiriki kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu ndiye aliyeibuka mshindi na kuondoka na cheki ya Sh. milioni 50.
Katika fainali hizo za kumsaka mwenye kipaji cha kuigiza ukumbini hapo, mshiriki kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu ndiye aliyeibuka mshindi na kuondoka na cheki ya Sh. milioni 50.
LULU AINGIA UKUMBINI
Shushushu wetu alimshuhudia Lulu akizama ukumbini humo akiwa amevalia gauni hilo lililoacha wazi sehemu ya mwili wake hivyo kujichafua mbele ya mamia ya mashabiki waliohudhuria.
“Yaani Lulu huwa anaonekana kama hajali vile, hebu muone nguo aliyovaa, imemuacha wazi sana, karibu mwili mzima uko wazi na anatangaza kwa kujiamini mpaka dah! Ni balaa!” alisikika mmoja wa wahudhuriaji hao.

upande wake, Lulu alionekana kujiamini kupita kiasi bila kujali macho
ya watu kwani alifanya kazi yake vizuri na hakuwa na wasiwasi wowote
kufuatia nguo aliyokuwa ameivaa mwanzo.
JOTI NAYE
Kufuatia kipaji alichonacho, Joti, kila mtu hakuamini pale alipopanda stejini kutumbuiza kwa staili ya aina yake kufuatia vazi lake alilokuwa amevalia yaani nusu mwanaume na kuwafanya watu washindwe kukaa na kuishia kuangalia shoo aliyokuwa akiitoa kwa mashabiki.

“Ama
kweli watu wana vipaji vyao, yaani kwa wakati mmoja Joti ameweza
kuigiza kama mwanamke na mwanaume. Ukiachana na hayo, hadi nguo nayo
imeshonwa hivyo! Dah! Fundi alifanya kazi tena nampongeza sana Joti
maana nilijua anakuja kuigiza,” alisikika mhudhuriaji mwingine.
Katika
maelezo yake, Joti alisema sababu ya kufanya vile ni sapraizi tu kwa
mashabiki wake kwani huenda walijua atakuja kama ambavyo huwa anafanya
sehemu mbalimbali.
“Nimeamua
kuja kivingine, hii staili ni ya kawaida tu, sema watu wameshangaa
kuniona vile, ndiyo maana Lulu alisema ni sapraizi kwa mashabiki, ni
kweli nimewafurahisha sana na huwa wanashindwa kunielewa kwa jinsi
ninavyobadilikabadilika,” alisema Joti.
Joti
hakuishia hapo kwani baada ya mshindi kutangazwa tu, alitoa shoo ya
nguvu huku watu wakimzunguka na kumuimbia kwa kufurahishwa jinsi
alivyokuwa akicheza.
Kabla ya shindano hilo, Lulu na Joti waliwahi kudaiwa wanatoka lakini kwa pamoja walikanusha vikali skendo hiyo na kuweka hadharani kuwa uhusiano wao ni wa kikazi tu.
Kabla ya shindano hilo, Lulu na Joti waliwahi kudaiwa wanatoka lakini kwa pamoja walikanusha vikali skendo hiyo na kuweka hadharani kuwa uhusiano wao ni wa kikazi tu.