http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/alikiba-akana-kuwa-na-beef-na-diamond.html
STAA
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Alikiba amekanusha kwamba ana ugomvi
na nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ kama ilivyokuwa
ikifahamika na wadau wengi wa muziki huo.
Akizungumza
katika kipindi cha Sporah Show kinachorushwa na Clouds TV, alisema hana
ugomvi na msanii yeyote kwani anajitambua na hawezi kuendeleza chuki na
wasanii wenzie.
Diamond
aliwahi kunikosea sana, lakini mimi kwa sababu sio mtu wa kukasirikika
niliamua kuachana nae na kufanya yangu, lakini nashangaa kila kukicha
nasoma kwenye vyombo vya habari kwamba nilimkosea, lakini kiukweli sina
ugomvi na mtu.
Katika
wimbo wake wa ‘Lala salama’, kuna sehemu niliweka vionjo vyangu baada
ya kunitaka nifanye hivyo, lakini cha kushangaza baada ya wimbo kutoka
sikusikia sauti yangu ila nilipoimba mimi akaimba yeye, kiukweli
nilijisikia vibaya, lakini nikaachana na hayo
alisema.
Alikiba
alisema maadamu anapenda muziki tena akiwa mpenzi wa nyimbo za Diamond,
anampongeza kwa mafanikio makubwa aliyopiga hadi kuing’arisha nchi
kimataifa ikiwamo katika tuzo mbalimbali.
Alikiba
ametamba na ngoma zake kama, ‘Dushelele’, ‘Cindelera’, ‘Mali yangu’,
‘My Everything’, ‘Single Boy’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na
kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA