BABA WA MAREHEMU KANUMBA AMFUNGUKIA MAMA YAKE NA KANUMBA Bongo news
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/baba-wa-marehemu-kanumba-amfungukia.html

BABA wa
aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba,
Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha
tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.Akipiga
stori na paparazi wetu, Baba Kanumba alisema anashangazwa na tabia ya
mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini Shinyanga
ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.
“Namshangaa
mama Kanumba ni njaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha ukoo wa
Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila sababu za
msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.
Akijibu
tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote aende
mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani mimi si
mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba
nilijiendea tu,” alisema.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA