Kashfa Nzito_VIGOGO WA CCM,YUMO WAZIRI MASELE ,WATAJWA KUPANGA NJAMA ZA KUMUUA DR SLAA NA MNYIKA MJINI SHINYANGA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/kashfa-nzitovigogo-wa-ccmyumo-waziri.html
Madiwani
walioasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamerejea na kudai
walirubuniwa na makada watano wa CCM kuhama kwenye chama hicho ili
wawatumie kuwaua, Dk. Willbrod Slaa na John Mnyika.
Madiwani
hao ni Sebastian Mzuka wa kata ya Ngokolo na Zacharia Martin Mfuko wa
kata ya Masekelo wote kutoka Shinganya mjini ambao wamewataja makada hao
kuwa ni Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana.
Wengine
ni Naibu waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele ambaye pia ni
Mbunge wa Shinyanga mjini, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC, chama
tawala, Nape Nnauye, na Habibu Mchange (aliyefukuzwa Chadema).
Wakizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama
hicho, madiwani hao walisema kuwa, mauaji hayo yalipangwa kutekelezwa
kwa kiasi cha Sh. milioni 180.
Diwani Mzuka alisema wamefika kwenye ofisi hizo ili kueleza kinachoendelea kudhoofisha chama na kuomba toba baada ya kuhama.
Alisema
mara baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuvuliwa madaraka
Chadema, Mchange alipewa kazi (dili) na CCM kutafuta viongozi na
madiwani wa Chadema lengo likiwa ni kukidhoofisha.
Alisema Mchange aliwafuata Shinyanga kuzungumza nao kuhusu suala hilo.
Alisema
Januari 27, mwaka huu alipewa kazi ya kulipua helkopta iliyokuwa
ikitumiwa na Katibu Mkuu Chadema, Dk. Slaa, Mbunge wa Ubungo, Mnyika na
Mwenyekiti wa kanda ya Mashariki katika ziara ya Kanda ya Ziwa.
“Aliniambia
kuwa Masele ana dili la shilingi milioni 180, baada ya ujumbe huo
nilipokea simu ya waziri huyo ambaye aliniambia nikifanikisha nitalipwa
fedha hizo,” alisema.
Alisema
kuwa Masele alimtaka aeleze helikopta hiyo itatua wapi, muda gani na
kama kweli wahusika wamo ndani yake kisha ulipuaji ufanywe na watu
walioandaliwa.
Alisema
alijiandaa na kufuatilia ila hofu ya kimungu ilimuingia akahofia taifa
litapokeaje tukio la kifo cha Dk. Slaa na yeye akihusika.
“Nilimweleza
Masele lakini alimpigia simu mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna Rose
Nyamubi, ambaye alimshauri kuwa sio vyema tukio hilo likafanyika
wilayani kwake, baadaye nilikutanishwa na katibu mkuu wa umoja wa vijana
ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda pamoja na mtu mmoja wa usalama, ”
alisema.
Aidha,
alisema aliwashauri badala ya kulipua watumie mabango na kurubuni
vijana kuhujumu ziara ya Dk. Slaa ambapo walifanikisha hilo.
Alisema
baadaye walikutana tena na Nape, Nchemba na kuombwa wawashawishi
madiwani na viongozi wengine wahamie CCM kwa ahadi ya kupewa ukatibu wa
Wilaya kwenye wilaya watakazoamua.
Alisema
baadaye madiwani hao walienda Mwanza mjini ambapo huko walikutana na
Nape ambaye alieleza kusikitishwa kitendo cha Chadema kumvua
uwanachama Zitto.
KUONDOKA CHADEMA
Alisema
Februari 26, mwaka huu waliondoka rasmi Chadema ambapo Nape alifika
huko na kukutana naye hoteli ya Kalena ambapo katika mazungumzo
alimhakikishia maisha mazuri pamoja na uongozi.
“Usiku
ulipofika gari la mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza iliwachukua na
kuwapeleka uwanja wa ndege na kusafiri kuja Dar es Salaam kukutana na
Nchemba ambaye naye aliwataka waelekee Dodoma na baadaye Kalenga,”
alisema.
Aliongeza
kuwa Dodoma walienda nyumbani kwa Kinana ambaye huko waliwakuta
Masele, Nchemba na Mchange ambapo wakati wote Katibu Mkuu alisifu
kitendo chao cha kuondoka Chadema.
Alisema katika mazungumzo makada hao walimwambia Nchange asichoke kwa kazi anayofanya.
ACT YATAJWA
Mzuka
alisema makada hao walikubaliana mgogoro ndani ya Chadema lazima
uboreshwe na kuahidi kugharamia fedha za kwenda mikoani na pia wakasema
kuna chama kitasajiliwa.
Pia
alisema makada hao walisema watahakikisha Msajili wa vyama vya Siasa,
Jaji Francis Mutungi anakipatia usajili wa kudumu kwa gharama yoyote
chama cha ACT ili CCM ipate ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema
katika mazungumzo hayo, Kinana alisema ACT imeanzishwa kwa lengo
maalum la kuipa CCM ushindi kwa kuwa hata huko duniani, ushindi wa chama
tawala unatokana na usajili wa vyama vipya.
WABUNGE WANNE KUHUJUMIWA
Makada
hao walikubaliana katika uchaguzi ujao mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu, asirudi bungeni kwa sababu ameitia hasara serikali kuhusu
hoja zake dhidi ya katiba.
“Katika jimbo la Lissu, ACT itafadhiliwa kusaidia kutoa mgombea CCM ambapo itagawa kura za jimbo,” alisema.
Diwani
huyo alitaja wabunge wengine ambao wapo kwenye mtego huo kuwa ni
mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema ambaye imeelezwa amesababisha
kushuka kwa utalii.
Wengine ni mbunge wa Iringa mjini Mchugaji Peter Msigwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi.
Kwa
upande wa Lissu alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa serikali za
mitaa, Diwani akijiuzulu anatakiwa aandike barua rasmi kwa mwenyekiti
wa Halmashauri na kuambatanisha na kiapo.
“Hawa
hawakufanya hivyo kwa hiyo bado ni madiwani wa halmashauri ya mji wa
Shinyanga,na uthibitisho kuwa hawajajiuzulu ni kuwa siku 90 zimepita
bila kutangazwa uchaguzi, “ alisema.
via nipashe
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA