TAZAMA PICHA ZA MAWE YA MWANZA YALIVYOPOROMOKA NA KUUA WATU WANNE.
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/tazama-picha-za-mawe-ya-mwanza.html
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.45 AM](http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.04.45-AM.png?resize=507%2C377)
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.53 AM](http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.04.53-AM.png?resize=508%2C375)
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.00 AM](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.00-AM.png?resize=502%2C371)
WATU
wanne wa familia mbili tofauti, wamepoteza maisha huku wengine wawili
wakijeruhiwa katika eneo la Sinai-Mabatini, Wilaya ya Nyamagana jijini
Mwanza baada ya kuporomokewa na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha
ikiambatana na radi usiku wa kuamkia Agosti 17,2014.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentine Mlowola, tukio
hilo lilitokea saa 8:55 usiku, ambapo mvua kumbwa iliyoambatana na upepo
wa wastani na radi nyingi ilinyesha na kusababisha majabali makubwa ya
mawe yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani mbili kuporomoka na kuziponda
nyumba hizo.
Aliwataja
waliokufa kuwa ni wanafunzi wawili wa shule ya msingi Mbugani, Kefa
Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12) kutoka katika familia ya Joseph
William yenye watu watano, huku mtoto Godfrey Joseph akijeruhiwa na
kukimbizwa hospitali.
Kamanda
aliitaja familia nyingine iliyoathirika kuwa ni ile ya Samson Odinya
ambaye alifariki pamoja na mkewe Kwinta Geko (24) huku mtoto wao, Betty
Samson (4) akijeruhiwa.
Tanzania
Daima lilifika eneo hilo, saa mbili asubuhi na kuushuhudia nyumba hizo
zikiwa zimesambaratishwa kabisa huku nyingine iliyo jirani jiwe likiwa
limejikita katikati.
Wakizungumza
na gazeti hili, baadhi ya majirani lisema kuwa nyumba zilizofikwa na
maafa zinamilikiwa na Joseph William na Lameck Ajiji.
Tukio hilo lilivuta lilivuta hisia za wakazi wengi wa jiji la Mwanza huku wengine wakishindwa kujizuia na kuangua vilio.
Mbunge
wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), alifika eneo la tukio kutoa pole
kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo,
ambapo alionesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna
kiongozi yeyote wa serikali aliyekuwa amefika eneo hilo.
Akizungumza
mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo, Wenje
alisema; “Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa.
Nitawasiliana na viongozi wa serikali na mchana nitarudi hapa tena.”
Mmoja wa
wananchi hao, ambaye ni Balozi wa shina namba 5 Mtaa wa Nyerere A,
Jackson Kitundu alisema kuwa tukio hilo linasikitisha sana, na kwamba
wanaomba viongozi wa serikali wasaidie kuwaondoa wananchi kwenye maeneo ya miamba.
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.07 AM](http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.07-AM.png?resize=508%2C378)
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.46 AM](http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.46-AM.png?resize=519%2C393)
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.53 AM](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.53-AM1.png?resize=514%2C378)
![Screen Shot 2014-08-19 at 9.06.36 AM](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/Screen-Shot-2014-08-19-at-9.06.36-AM1.png?resize=536%2C396)